Inashangaza kuona watu wanambiwa na kupewa ahadi kuwa wataondolewa
umaskini na kuwafanya wawe na maisha mazuri. Umaskini wanaouongelea
waheshimiwa ni umaskini upi?kuna umaskini wa fikra, umaskini wa njaa,
umaskini wa hela, na umaskini wa elimu,sasa waheshimiwa wakisimama
kuwapigia watu tarumbeta ya kuleta mabadiliko na kuondoa umaskini mbona
hawaelezei namna na jinsi watakavyo mfanya kila mtanzania aondokane na
umaskini wa aina zote zilizotajwa hapo juu?inawezekana ukawafanya
watu wote nchi hii wakawa kweli matajiri au ni siasa inayosukuma hayo
mambo kuliko utawala wa akili na kufikiri juu ya hao waheshimiwa
wayasemayo?Hata nchi zilizoendelea bado zina maskini,inakuwaje sisi Leo
tuambiwe kuwa baada ya uchaguzi tunakuwa matajiri bila hata ya
kuonyeshwa ishara halisi kimatendo ila kwa maneno ndo kwingi?Hayo yote
ni kuongelea mdomoni kuliko kongelea akilini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni