Itawezekana kupata mabadiliko ikiwa wanaodai hayo mabadiliko hata wao
wenyewe hawajajiletea mabadiliko hata kwa mambo madogo waliyonayo?mfano
kama mtu anadai mabadiliko wakati hata magugu yaliyozunguka nyumba yake
yanamshinda kuyangoa, mtu akishindwa kufagia nyumba yake na kuipanga
vizuri na hata akashindwa kupanga chumba chake anapolala mwenyewe sasa
ukisikia huyo anadai mabadiliko huyo kweli anadai mabadiliko kutoka
ndani ya moyo wake au ni msukumo wa mikumbo ili mradi siku
imeenda?Itawezekana kweli kudai mabadiliko ihali mdai mabadiliko
hajajibadilisha na kubadilika na hatimaye kudai ili abadilishwe
zaidi.Kamwe haitowezekana mabadiliko kwa watu kama watu wenyewe
hawajajibadilisha katika vitu vifuatavyo:1.Kujibadilisha kifkra
2.Kujibadilisha kimtizamo hasa juu ya kufikiri,kutenda, na kuchukulia
uhalisia wa mambo.3.Kujenga mtizamo chanya na kujikubali mapungufu
4.Kuondoa dhana ya kujihisi wanyonge daima na hivyo kujenga dhana ya
kuwa wategemezi daima. Kwa hili ni kuwa dhana ya kutegemea kila kitu
kupewa ndo wengi tumejikuta tunaitwa mbumbumbu na hivyo kutengeneza
mwanya kwa waheshimiwa kutoa ahadi hewa za mabadiliko
yasiyokuwepo.Tusipojibadili namna ya kuchukulia na kufanya mambo
tutajikuta hatuna mabadiliko kamwe.Haiwezekani ukalala bila ya kufanya
lolote na hapo ukategemea mabadiliko yatokee.Kuleta mabadiliko ni moja
ya mapinduzi katika historia.Tukumbuke kuwa hustoria ni kwa wale tu
waitengenezayo(history is only for those who make it,never sleep and
expect history to be made for you).Mabadiliko yatakuja pale ambapo
tulisha anza sisi wenyewe kwa Yale madogo tuliyoanzisha kwa juhudi zetu
wenyewe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni