Ahadi yaweza kuleta matumaini ya kuishi kwa muda mrefu bila ya kuona
ukweli wenyewe au uhalisia wa hiyo ahadi.Kwa kifupi naweza sema ahadi
siyo tofauti na ndoto maana hivyo vyote ni ishara zinazolenga kwenye
uhalisia japo zenyewe siyo uhalisia(reality)kamwe. Ahadi ni kama vile
mtu kusikia harufu ya chakula kikipikwa au kukaangwa akasikia kushiba
kumbe ihali bado ana njaa ya kutosha. Sasa wengi wetu ndo hali
tuliyoifikia wakati tukielekea uchaguzi mkuu.Hivi hizi ahadi
zinazotolewa na waheshimiwa tukapiga makofi kwa nguvu tukafanana na
waliokwisha kula na kushiba, hivi huu ni ukweli na uhalisia au bado tuko
kwenye ndoto?.Kuna namna nyingi zakudanganywa na ukakubali kiulaini
bila ya manunguniko.Njia mojawapo ni ahadi ambazo ni nusu ya uhalisia na
nusu uongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni