Tujiulize swali la msingi kuwa kama walimu wetu wangelikuwa wanalipwa
posho kama za wabunge kwa mwezi kungelitokea nini katika sekta ya
elimu?Hivi huyu anayeenda kuwakilisha wananchi katika chombo cha dola
ambacho ni moja ya mihili mikuu ya serikali kimaarifa au kielimu huyu
inasemwa kuwa walau awe na elimu ya kidato cha nne na zaidi ajue kusoma
na kuandika basi. Cha kushangaza na kuchekesha ni kuwa huyu ambaye
anasemwa kuwa ajue kusoma na kuandika mara nyingi huwa tunawaona kupitia
Luninga wakiwa wamechapa usingizi na kusahau kile kilichowafanya wawe
hapo;kisa ni kujua kusoma na kuandika na mwishowe huyo anapata posho
Mara nne au tano ya mwalimu au mtu yeyote mtaaluma ambaye kila siku
lazima asumbue kichwa chake kufanya kazi Fulani,wakati waheshimiwa
wanalala na posho inaingia.Hivi ninani ambaye hawezi simama pale bungeni
na kutoa hoja? kusimama pale kunahitaji kuumiza vichwa kweli?jibu ni
hapana ila kukaa pale ni sawa na kusema kama waswahili wa mtaani
wasemavyo"kula kuku kwa mrija." Hii itakuwa sahihi nikisema kuwa baadhi
ya wataaluma wetu hasa maprofessa wetu wa vyuo vikuu wanaacha fani zao
na kukimbilia kwenye siasa maana huko kuna ulaji kwa njia ya mtelemko
bila ya kusumbua vichwa.Hivi kama hao wanaokimbia fani zao na kuingia
katika siasa wangelikuwa wanapewa keki wanayopewa hawa waheshimiwa
bungeni tungelikuwa hatua ya juu sana kielimu. Uwezo wa kujenga hoja na
fikra hautegemei kusoma na kuandika,Bali unahitaji pia nguvu ya
kufikiria na kujenga hoja makini.Wale waliopaswa kushauri wanaoongoza
pia nao wanataka kuongoza,je hapo nani atatoa maoni na ushauri kwa
wanaoongoza?matokeo yake ni kuishia katika ushabiki usiojenga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni