Jumanne, 11 Aprili 2017

UKIKUTANA NA CHANGAMOTO MSHUKURU MUNGU, MAANA NI NDANI YA HIZO CHANGAMOTO UNAPATA FURSA ZA KUVUMBUA SULUHISHO LA HAYO MATATIZO

Watu katika ajira ziwe ni ajira za serikali au ajira za mashirika binafsi yasiyo ya serikali huwa daima katika utendaji wao huwa wanapata kuhamishwa kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine cha kazi na wakuu wao wa idara. Katika kuhamishwa kwa mfanyakazi kutoka kituo kimoja kwenda kingine huwa daima sababu zifuatazo zinapelekeaga kuhamishwa kwa mfanyakazi Fulani:
1.Amehamishwa kwa kuwa ameonekana kuwa mtendaji mzuri hivyo aende akatende vivyohivyo katika eneo kingine... ambalo halina mtendaji mwingine mzuri kama huyo.
2.Ni mtendaji mbaya, ni mzembe, hivyo hilo eneo alipo hafai kufanya kazi aliyopewa, kwa maana kwamba huyo hasipohamishwa ataendelea kuharibu kazi ya serikali au kampuni, ni kwa msingi huo uhamisho wa namna hii huambatana na kubadilishiwa kazi baadala ya kuendelea na kazi hiyo hiyo.

3. Uhamisho ambao matokeo yake ni mgogoro/kutohelewana kati ya mwajiri/kiongozi wa idara na mwajiliwa. Daima mwajiri/kiongozi wa idara akiona kuwa mwajiriwa wake anakuwa mwerevu kumpita au hawaelewani kwa mambo Fulani kati yao, mwajili kwake hufanya kitu kidogo ili kuondoa huo mwiba ulio nyayoni mwake(mwajiriwa) Afanyacho kiongozi huyo ni kumpa uhamisho huyo mwajiliwa kwa kumpeleka maeneo ambayo huyo mwajiliwa hatoridhishwa nayo na hivyo anaweza acha hiyo kazi(akufukuzaye hakwambii toka).
Kwangu ni kwa hiyo namba tatu, kwamba kama anayehamishwa anapewa uhamisho kama adhabu, hana budi kufurahi na kushangilia maana anavyohamishwa kupelekwa mazingira magumu/hatarishi ndoo vivyo hivyo atatumia akili yake, uweza wake, na ujuzi wake kujifunza namna ya kupambana na hali ngumu. Tena faida kwa huyo ni kwamba aweza kuwa na ujuzi zaidi hata kumpita yule aliyemwamisha kituo cha kazi. Daima ukihamishwa mshukuru aliyekuhamisha hata kama ilikuwa kwa lengo baya,maana kwa jinsi hiyo anakuongezea weredi wa kufikiri na kuwa na ujuzi mpya katika kuona mazingira hatarishi kama moja ya fursa za kukusaidia kutenda vyema na kujifunza zaidi kutoka katika mazingira yaonekanayo hatarishi kwake.

NDANI YA GIZA HUWA NDOO TUNAPATAGA SULUHISHO LA KUTENGENEZA MWANGA

Ukipata kuona kuwa giza limetawala sana bila ya kukucha, basi fungua dirisha la imani yako na tafakari haya: Nyota huonekana vyema katika usiku wa kiza. Vivyo hivyo ni ndani ya dimbwi la matatizo huwa ndoo tunapata fursa za uvumbuzi, kujifunza na kutatua matatizo.

MATUMIZI MABAYA YA SILAHA ZA MOTO

    Tanzania kumekuwepo utaratibu wa kupewa kitambulisho kwa kila raia.
    Lakini cha ajabu nimeona katika habari mmoja alivyoulizwa atoe kitambulisho chake, akatoa bastola! Kumbe hizo bastola ndoo vitambulisho vipya vilivyoidhinishwa?

BINADAMU DAIMA HAKOSAGI KISINGIZIO

    Apambanaye ili ale keki akaikosa daima huishia kulaumu kuwa keki ni chanzo cha ugonjwa wa sukari, hivyo huishia kula viazi kama mbadala, ila akiitiwa ale hiyo keki hutupa viazi pembeni na kukimbilia hiyo keki aliyoituhumu hapo kabla kuwa ni chanzo cha ugonjwa wa sukari.