Jumanne, 20 Oktoba 2015
UCHAGUZI MKUU UMETUFIKIRISHA NINI?
Tunavyokaribia kufanya uchaguzi mkuu baadhi ya mambo yanajitokeza ambapo
kabla ya hapo mambo hayo yalikuwa hayajajitokeza japo yalikuwepo
kiukimyakimya.Mfano ahadi lukuki zilikuwa hazizungumziki na hao
waheshimiwa, kwa kipindi hiki cha uchaguzi ni kipindi ambapo wapiga
ramli wanavuna vya kutosha.Nikipindi ambapo ikiwezekana wachawi
watagundulika.Tukiendelea zaidi tunaona kuwa kila mmoja anamlaumu
mwingine kwa kutokutimiza wajibu wake.Hivi katika kulaumiana ninani
alaumiwe?yule aliyepewa dhamana na chama
chake awe mtendaji wa serikali au chama chenyewe?Imezoeleka kusikika
chama Fulani kinalaumiwa kwa utendaji,je ni halali kulaumu chama au
watendaji wake?Maana kikilaumiwa chama maana yake ni kuwa wanalaumiwa
wanachama wote kuanzia ngazi ya kitongoji hadi taifa kwa ujumla wake,
kuna uhalali gani wa kumlaumu mwanachama asiyejua nini linatendeka na ni
mipango gani inaendelea kwenye chama chake? Kwa msingi huo tunaona
wengi wa wapiga campaign wakiwania ile keki nzito hutumia nafasi hiyo
kulaumu chama na wanachamawake wote baadala ya kuelekeza tuhuma kwa
watendaji.Mbegu hiyo hupandikizwa kwa watu nao watu huamini kuwa chama
ni kibaya.Huo ni mchezo wa siasa ambao hutumika kuwafanya wananchi
waamini visivyo.Mchezo wa siasa ni mchezo daima ambao wengi huuita
kuchafuana(mchezo mchafu).Hivyo kuchafuana katika siasa huwa kunajumisha
kuwachafua wote bila ya kuangalia ninani mhusika zaidi ya wote katika
kundi.Katika lugha na maongezi ya kifalsafa na lugha ya kifalsafa
kuongea kwa ufahamu wa namna hiyo(reasoning) huitwa "Fallacy of
generalization),yaani kuacha kuongelea jambo husika au mhusika na
baadala yake wanashambuliwa hata wasiohusika kamwe.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni