Ni jambo la kushangaza kuona watu wanatawaliwa na hisia(feelings) za
wengine na kuzifanya hisia zao.Kimsingi kundi la watu wa namna hiyo
linakuwa limepoteza malengo na mwelekeo kwa ujumla katika
maisha.Ukiangalia ushabiki unaofanywa kwa sasa katika vyama vya siasa
unaweza tambua kuwa sio mashabiki wote wanajua walitendalo ila wengi wao
huenda kwa mkumbo wa kwa kuwa Fulani kashabikia hebu na Mimi nishabikie
kitu ambacho ni hatari katika maendeleo na utu wa kila mmoja wetu.Hivyo
hatuko mbali kusema kuwa ushabiki ninamna ya watu kuishi maisha ya
wengine ili mradi siku ipite.Ushabiki lazima uwe na tija na malengo pia
ya kumnufaisha mwananchi kuliko kumnufaisha mgombea.Ni heri kutoshabikia
yale tusiyoyajua maana wanaofaidika ni wengine.Kwa jina la ushabiki
wengine wameshanunuliwa kwa kilauri/kiloba wakiwa wamesahau kuwa wanauza
utu wao na haki zao kwa vitu vya mpito visivyokumbukwa daima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni