Matumizi ya lugha isivyo hitajika yaweza kupoteza ukweli wa mambo
kihalisia na kufanya hata watu wasiohusika hata vitu visivyoweza kutumia
ufahamu(reasoning) kuonekana kuwa vina hatia. Mara nyingi tumeshuhudia
mfano ajali nyingi hapa kwetu na duniani kote.Ajali kama hizo
zimehusisha watu kupoteza maisha kutokana na hizo ajali. Mfano
tumeshuhudia ajali za vyombo vya moto kama vile pikipiki na magari,
ndege,na vinginevyo. Jambo ambalo huwa daima linanishangazaga ni kwenye
mawasiliano wakati wa kutoa taarifa
baada ya kutokea ajali mfano utasikia mtu anaongea kuwa " nimeangushwa
na pikipiki,au nimeangushwa na gari" hivi kweli hii inawezekana
kimaongezi kuwa mtu ameangushwa na pikipiki au gari? mimi naona kuwa
hiyo siyo sahihi kamwe.Daima mtu huwa ndo anaiangusha pikipiki au gari
maana hivi vifaa vya usafiri huwa havina akili au utashi wa kuamua
kumdondosha mtu bali uzembe wa mtu huwa ndo unamfanya adondoshwe au
aangushwe na hicho kifaa cha usafiri.Hiyo ndo kawaida yetu binadamu kuwa
huwa hatupendi kuwajibika kutokana na uzembe wetu baadala yake ni
kuhamishia maumivu na hisia kwa watu na hata vitu visivyo na uhai
kuhusika na mikosi tuipatayo. Nimesikia mara nyingi mtu mmoja akisema
kuwa kamwe hatopanda pikipiki, nilipomuuliza sababu ya kusema vile
akaniambia kuwa ni kwa kuwa pikipiki zimeangusha na kuua watu
wengi;swali langu kwake lilibaki kuwa " je pikipiki huwa inaangusha mtu
au mtu huwa ndo anaiangusha?" Uwajibikaji ni muhimu kabla ya kuelekeza
tuhuma kwa wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni