Ukitaka kutambua utu wa mtu na kumjua yeye ninani mpe Uhuru wa umfanyie
nini?hapo ni dhahiri kuwa utapata majibu mengi kutoka kwa huyo mtu juu
ya analotaka umfanyie hata kama mengine yapo juu ya uwezo wake.Katika
nafasi hiyo utapata kutambua kama huyo mtu ni mchoyo na pia mwenye uchu
wa kutaka kutawala au pia utapata kujua unyenyekevu wa huyo mtu kadiri
ya kitu ambacho amekuomba ukamfanyie.Sasa tuje ngambo nyingine ya
Shilingi ambapo Leo hii tumeshuhudia wale waliokuja kutuomba
dhamana ya kuongoza nchi.Wao wakati wanahangaika ili tuwape dhamana ya
kutuongoza mambo yamekuwa kama ifuatavyo:1.Wao wamekuja na bado wanazidi
kuja kwetu na tumewauliza "je mwataka tuwafanyie nini?" Wao wakajibu
kwa sauti kubwa "mtupigie kura ya ndiyo katika uchaguzi mkuu
ujao."2.Pindi na sisi ilipokuwa zamu yetu juu ya wao watufanyie nini,
wamekuja na majibu mbalimbali yenye kutia moyo japo hayana uhakika
asilimia mia moja.Moja ya majibu mepesimepesi ni kufuta baadhi ya Kodi,
Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.Kuanzisha viwanda,
kuhakikisha kuwa vijana wote(waliosoma na wasiosoma)wanapata ajira na
wanakuwa na maisha mazuri n.k.Hayo yote ni mazuri sana ila wengi wetu
tunasahau kuwa siyo kila ahadi utekelezeka! Kwa Mawazo yangu ni kuwa
itakuwa rahisi kwetu kutoa majibu ya maswali yetu ya tuwafanyie nini
waheshimiwa maana majibu yanaeleweka, kuwa tutawapigia kura ya
ndiyo.Wasiwasi unakuja kwa majibu ya maswali yetu kwao kuwa watatufanyia
nini?majibu yao kwetu yamekuja na ahadi ambazo ni vigumu kuamini kuwa
zitatekelezeka.Tunasahau kuwa Siasa ni mchezo ambao siyo wote twaweza
kuucheza. Punde tutashuhudia kama tulidanganywa juu ya hizo ahadi au la!
wakishapewa hayo majukumu ndoo itakuwa kutekeleza au kutokuteleza hizo
ahadi.Hofu yangu ni kwamba kwa nchi kama Tanzania,Ahadi zilizotolewa
baadhi ziko nje ya uwezo wake, kama vile Elimu bure na ajira kwa kila
mtanzania hasa vijana.Hayo yote ni majibu ya tutafanyiwa nini.Yatubidi
tufunguke macho na kuelewa kati ya kuambiwa ukweli au kulaghaiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni